Msanii wa bongofleva, Nay wa Mitego

Pata kujua ni nini kilichoendelea kati ya msanii Nay wa Mitego na Marco Chali.

Hii post itakuhusu sana kama uliisikia ya producer Marco Chali na msanii Nay wa Mitego kwamba hawapatani.

Kwenye dstv.com Nay ameongea rasmi kwamba hakuna ubaya au chochote kati yao kwa kusema: "Mimi na Marco tunaongea, tulishawahi kutofautiana kidogo sababu ya kazi, Marco Chali ni mmoja kati ya watu niliofanya nao kazi sana."

Kama wataka muziki ya kupendeza basi jiunge na DJ Tass kwenye Wakilisha, Jumatatu hadi Ijumaa, saa 17:00 kwenye Maisha Magic Swahili.

"Tunaheshimiana, unajua sisi ni binadamu kwenye kutofautiana tunatofautiana, kweli inafika time mnatofautiana, ilitokea katikati hapo maswala ya kazi sababu kila mtu ana hili na hili kwahiyo kidogo maelewano lazima yawe magumu."

Nay aliendelea kusema: "Mimi na Marco sasa hivi hatuna tatizo, ni brother kwangu na ninamuheshimu... matatizo yaliyokuwepo yameisha na lolote likitokea tutafanya kazi pamoja."

Kwenye sentensi ya mwisho Nay amegusia kidogo kama exclusive kwa dstv.com kwamba mwezi wa sita 2015 Mungu akijali atakua ameshahamia kwenye nyumba yake mpya ya kifahari aliyoijenga kutokana na muziki.