Msanii TID kutoka Tanzania

Mkongwe katika game ya bongoflevani tangu kitambo TID ambae kwa sasahivi amejikita zaidi kwenye muziki wa live band perfomance.

Kutana na wasanii kutoka Tanzania kwenye kipindi cha mziki cha Mzooka kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

TID amezungumzia tasnia nzima ya game ya bongofleva kwa sasa akidai kuwa uhalisia umepotea sio kama kipindi kile alivyokuwepo kwenye game kwa sababu wasanii wengi wa sasa hivi wanaiga sana muziki wa nje.
 
Amesema, "Uhalisia wa muziki wa bongofleva umepotea. Watu sasa hivi wanataka kuimba kama Wanigeria, watu wanataka kuiga vitu vya nje lakini wakumbuke kwamba bongofleva maana yake ni mchanganyiko wa muziki wa hip hop na RnB."
 
TID pia alielezea sababu yake iliyomfanya akaandika wimbo wa Confidence, "Niliamua kuandika wimbo wa Confidence ili kuwaonyesha vijana wanatakiwa kufanya nini kwenye nyimbo zao."
 
TID alimalizia, "Ni mara chache sana kwenye tuzo zetu kushuhudia tuzo za heshima zinatoka kwa 'Legends' wa muziki wetu kutambua mchango wao, hata aliyeanzisha tuzo za muziki za Killimanjaro marehemu James Dandu sijashuhudia akipewa heshima yake tuzo hizi zinapofanyika."