Msanii Tunda Man kutoka Tanzania

Tunda Man ataja idadi ya ngoma atakazoziachia 2017

Mkali wa mda mrefu kwenye game ya bongofleva ambae anaendelea kudunda mpaka hivi sasa na hit song yake aliyoiachia January 2017 Debe Tupu si mwingine bali ni Tunda Man.

Burudika na Debe Tupu kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.

Hit maker huyo kutokea Tip Top Connection amefunguka na kuweka wazi mafanikio anayoyaendea kwa mwaka 2017 kwa kutaja idadi ya hits atakazotoa mwaka huu 2017 kwa kuwaweka mashabiki tayari kuzipokea.
 
 
Tunda Man amedai ndani ya mwaka huu ataachia nyimbo 5 pamoja na video zake.
 
“Namshukuru Mungu mwaka umenza vizuri na ratiba yangu ya mwaka au kalenda yangu imepangika vizuri. Nitaachia nyimbo tano pamoja na video zake, sitaki mwaka huu kutoa ngoma chache kwa sababu muziki wa sasa umebadilika mashabiki wanataka kazi nyingi zaidi,” alisema Tunda Man.
 
Aliongezea, “Kwa hiyo kazi zipo nyingi, kuna ngoma nimefanya na Yamoto Band, kuna wimbo nimefanya na Jaguar wa Kenya, yaani kuna kazi nyingi Mungu akitujalia ngoma tano zitatoka mwaka huu.