Tarsisi na Bella

Msanii Tarsisi Masela akutana na DStv na kujibu ikiwa anamuiga Christian Bella au la kwenye single yake mpya.

Ni mwimbaji kutoka kwenye band ya Akudo IMPACT ambaye amefanya kazi kwa zaidi ya miaka 6 akiwa nayo hapa Tanzania akitokea kwao Congo DRC.

Tarsisi Masela ameongea kwenye dstv.com kuhusu single yake mpya inaitwa Usingizi, akisema pia imefanya wengi wamuulize au kuona kama inafanana au kupita kwenye njia za Christian Bella ambaye alikua rais wake Akudo kabla hajaondoka.

Kupata burudani ya video kali kutoka bongo, tazama kipindi cha Mzooka unayoletewa kwenye channel mpya Maisha Magic Bongo (DStv Channel 160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.

Kwenye majibu yake, Tarsisi amesema, "Mimi simuigi mtu yeyote labda yeye ndio ananiiga, mimi ndio niliwahi kuja Tanzania na nikampokea alivyokuja.... mimi nafanya kivyangu tu siigi mtu."

Amesema hakasirishwi anapoulizwa hivyo kwa sababu Bella ni binadamu kama yeye, akichukia kufananishwa nae ni kama ushetani ila anataka ifike mahali watu waendelee na maswali mengine na sio kuendelea kuuliza hichohicho kila wakati.

Masela ambaye ameomba likizo Akudo ili kupumzika na kuendelea na shughuli zake ndogondogo, amesema sababu kubwa za kuifanya single ya 'Usingizi' bila kumshirikisha mtu, ni kukwepa maneno ya watu kusema kwamba amebebwa.