Msanii wa Tanzania Alikiba

Alikiba anajulikana kama vocalist mzuri katika bongofleva na amefanya vizuri zaidi kwa mwaka huu 2016 ambapo hit song yake Aje imemletea mafanikio makubwa.

Alikiba ameeleza kuwa hivi karibuni hatatoa hitsong nyingine yoyote akidai kuwa atapata hasari wakati bado Aje inafanya vizuri sokoni.
 
Burudika na hit ya Alikiba ya Aje kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.
 
King Kiba alisema haya, “Naamini mimi muziki wangu una thamani kubwa sana ndio maana nyimbo zangu zinakaa muda mrefu sokoni."
 
Alieendelea, “Kwahiyo bidhaa yangu inavyokaa muda mrefu sokoni siwezi kuleta bidhaa nyingine kwa sababu hii ya kwanza haijaisha, nataka watu wapate watosheke ili wakiridhika niweze kutoa nyingine kwa sababu nitapata hasara kama nitatoa bidhaa nyingine ambayo itakuwa nzuri kuliko ile ambayo ipo sokoni."
 
Alikiba aliongeza kuwa remix ya wimbo Aje ipo tayari ila kwa sasa hawezi kuitoa kwa kuwa anazipa muda kazi ambazo zimetoka akiwa ameshirikiana na wasanii wenzake.