Msanii Christian Bella na Alikiba

Nashindwa ya Christian Bella na Alikiba sio wiki hii tena

Najua mashabiki wengi wa muziki Tanzania walishaiweka tayari mikono miwili kwa ajili ya kuipokea single mpya ya Christian Bella na Alikiba iitwayo Nashindwa lakini taarifa za uhakika ni kwamba hii single haitotoka wiki hii tena.

Management ya Alikiba imesema single hii itatoka ijumaa ya wiki ijayo na imebidi iwe hivyo sababu Christian Bella amesafiri, hivyo itabidi asubiriwe kwanza ili waje waanze kufanya media tour pamoja.
 
Ukiendelea kungoja single hii, burudika na single zingine kem kem kama Chekecha Cheketua ya Alikiba kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00
 
Pamoja na kwamba single yenyewe haijatoka, stori ya single yenyewe inatajwa kama movie, yani ni kama mrembo ambaye Bella amempenda alafu kumbe ni mpenzi wa Alikiba ila Ali baada ya kujua mrembo wake anapendwa na Bella hakutaka kusema chochote mpaka aone mwisho wake utakuaje.
 
Video ya single yenyewe imefanywa Afrika Kusini na inatarajiwa kuwa video ya kuchezwa sana kwenye TV kutokana na muonekano wa kitofauti na video nyingine za Watanzania.
 
Christian Bella yuko nyumbani kwao Kinshasa wakati Alikiba amesafiri kuelekea nchini Marekani kwa ishu zake za ubalozi wa kulinda tembo pamoja na ishu nyingine za kimuziki.