Msanii wa bongofleva Shetta

Pata kujua kwa nini msanii wa bongofleva Shetta kaongeza bei kwa mapromota.

Jina lake lipo kwenye playlist ya radio na TV kwa kiasi kikubwa baada ya hit single yake ya Shikorobo aliyofanya na msanii Kcee wa Nigeria.

Anachosema Shetta kwa sasa ni utaratibu wake mpya wa kutokea kwenye show manake jina limeongezeka na hata kiwango anachotoza nacho ameongeza.

Burudika na muziki wa Shetta na wasanii wengine kwenye kipindi cha Official African Chart kila Jumanne saa 21:00 kwenye MTV Base. 

Amesema, "Zamani nilikua na bei ndogo kidogo kama milioni 5 au nne lakini sasa hivi nimeongeza mpaka milioni 8 mpaka tisa, nimefanya hivyo sababu hata jina langu limekua kubwa sasa hivi na mimi mwenyewe nimekua mkubwa."

"Promota ni lazima wanilipe pesa ambayo inahitajika japo watu nikiwaambiwa wanashtuka ila ukweli ni kwamba haiwezekani kubaki kwenye bei ile ile," Shetta kasema.

Shetta anajipanga kwenda Nigeria pia kufanya media tour sababu hii ni single yake ya pili ambayo inapata nafasi ya kuchezwa sana kwenye radio ambapo ya kwanza ilikua ni Kerewa ft. Diamond Platnumz.