Shetta

DStv.com inae msanii wa bongofleva Shetta kwenye hii nafasi, single yake ya mwisho kuiachia ilikua Shikorobo ambayo ilimpa headlines na kuifanya iwe miongoni mwa kolabo zilizobamba featuring Kcee wa Nigeria.
 
Umaarufu wa Shetta umezidi kuongezeka tofauti na miaka minne au mitano iliyopita na yote hiyo ni kutokana na uwekezaji anaoufanya kwenye muziki sasa hivi.

Patana na Shetta kwenye show ya Mzooka saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo kila Jumatatu hadi Ijumaa.

Kitendo cha yeye kufuta picha zake zote Instagram kumemfanya apokee maswali mengi sana ambayo amekubali kuyajibu kupitia DStv.com kwa kusema 'Management yangu tulikaa kwenye kikao cha mwisho, tumejaribu kuwa kivingine na moja ya vitu management yangu imeniambia ni inabidi niwe tofauti na miaka iliyopita'
 
"Kufuta kwangu picha kumezua maneno ila ukweli ni kwamba nataka kumtengeneza Shetta mwingine, kuna kitu nimepanga kukifanya hivyo watu wasubirie tu ila hata jina langu instagram nimelibadilisha, ni Official Shetta na sio Shetta TZ tena".
 
Kitu ambacho nataka kukifanya sasa hivi ni kuisikiliza sana management yangu, nataka kubadilika na kufanya biashara zaidi kama brand inayojitegemea, kutengeneza brand kunahitaji kujipanga, ndio ninachokifanya.