Msanii kutoka Tanzania Shetta

Karibu tena DStv.com ambapo hapa utakutana na stori nyingi za mastaa wa bongo Tanzania na maisha yao, kwa leo tunae Shetta, mkali mwingine wa bongofleva ambaye njia yake kufika juu haikua rahisi ndio maana ikamlazimu mpaka kufanya kazi za nyumbani.

Nurdin Bilal Ali ndio jina lake halisi na anazo hits kama kerewa na Shikorobo chini ya producer Jobanjo, leo Shetta ameelezea maisha aliyopitia kabla hajatoka kwenye muziki wa bongofleva.

Mpate Shetta kwenye show ya mziki bomba ya Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Shetta amesema, "Nimehangaika na vitu vingi, tunakutanana changamoto nyingi. Tunaenda studio hatuna pesa ya kulipa, ilishawahi kuishia na msanii alikuwa mkubwa sana kwa kipindi kile nilishawah kuosha gari lake, wakati mwingine namuogesha hata mdogo ake na vyombo pia."

Shetta ameongelea kuwa sio rahisi kutoka kama watu wanavyodhani ila nimengi wasani wanapitia magumu ambayo hata yeye binafsi amepitia mpaka kufikia malengo.

Ameendelea kusema, "Nishawahi kuosha vyombo, nishawahi kufanya kazi zote ambazo kipindi kile zilikuwa zinaonekana kuwa aibu kuzfanya lakini kwa vile nilikuwa na malengo yangu nilijua nini nataka kwenye maisha yangu na ndoto yangu ilinibidi tu nizifanye na leo nimefika hapa."