Msanii wa Tanzania Shaa

Msanii wa Tanzania Shaa apata airtime kwenye MTV Base na wimbo wake mpya Toba

Rekodi ya Watanzania kupata airtime kwenye TV stations kubwa za Afrika inazidi kuvunjwa. Hii ni kutokana na mabadiliko kwenye utengenezaji wa video zenye ubora.
 
Mwingine ambaye tunae leo kwenye kwenye list ni mwimbaji Shaa ambaye amezichukua headlines kwa video yake mpya ya Toba ambayo sasa itachezwa kwenye MTV Base, DStv Channel 322.
 
Ungana na Shaa na wasanii wengine kutoka Afrika Mashariki kama Sauti Sol kwenye kipindi cha Best of Spanking New, kila Jumatano saa 23:00 kwenye MTV Base.
 
Msanii huyu Shaa alikuwa mojawapo wa mentors kwenye show ya Maisha SuperStar ilikuwa kwenye Maisha Magic miezi sita. Mafans walipata kumjua Shaa kwa vilemba katika show hii. Yeye pamoja na Ay waliwakilisha Tanzania katika show him bomba!
 
Wengine wanaopata airtime MTV Base ni pamoja na Vanessa Mdee, Navvy Kenzo, Joh Makini, Jux, Diamond, Ali Kiba na Yamoto BAND.