Msanii Shaa kutoka Tanzania

Staa mwanadada kutokea bongoflevani mkimfahamu kama Shaa ni miongoni mwa wasanii wakike wanaofanya vizuri  kwenye game ya mziki Tanzania.

Baada ya ukimya, Shaa ameongea na DStv.com na ameelezea mipango yake ya kusaini na kuwa na wasanii wake binafsi hivi karibuni. "Mimi mipango yangu kwa mwaka huu kwanza ni mimi maana mwaka ndo unaisha huu."

Aliendelea, "Lakini mipango yangu kwa mwakani sasa 2017 tayari kuna wasanii watatu ambao nilikuwa nawamendea nanikawa approach na msanii mmoja nshampata mtamsikia ni kijana mmoja kutoka Tanga. Na mwingine ni Mayra kama mnamkumbuka alikuwepo kwenye shindano la maisha super star na yeye tutafankisha kazi zake mwakani , so kwa kuanza tu mwakani SK MUSIC itakuwa na hao wasanii wawili so nitawatambulisha rasmi na vitu vyote kama hivyo."

Kutana na Shaa kwenye show ya Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.