The cast of Doc McStuffins

Disney na MultiChoice watangaza kuileta Disney ya Kiswahili kwenye DStv

Ni ripoti kutoka hapa Mauritius kwenye tamasha la MultiChoice Africa Content Showcase ambalo limekutanisha waandishi wa habari na watangazaji kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuwaonyesha na kuwapa vitu vipya kutoka MultiChoice.

 
Channel ya Disney ambayo inapatikana kwenye bidhaa ya DStv imetangaza kuizindua katuni maarufu inayopendwa na watoto ya Doc McStuffins kwa lugha ya Kiswahili ili kupata utazamaji mkubwa zaidi kwa wanaotumia lugha hiyo upande wa Afrika Mashariki na kati.
 
 
Kupitia DStv Channel 309 ikiwafikia zaidi ya watoto milioni 1.3 barani Afrika kila siku, kwa ujumla channel hii sasa inazifikia nchi mia moja kumi na moja ikiwa ndani ya tafsiri ya lugha 16.
 
Mbele ya waandishi wa habari hapa Mauritius, uongozi wa channel hii umesema kuongezea Kiswahili kwenye tafsiri kutasaidia kuongeza idadi ya Watazamaji hasa ikizingatiwa kwamba kwenye nchi zenye kutumia kiswahili kuna utazamaji mkubwa vilevile.