Bongo star Roma

Roma Mkatoliki ni msanii anaefanya Hiphop Tanzania na anafaanya vizuri kwenye game hii kwa michano mikali.

Rapper Roma amedondoka kwenye Dstv.com leo ambpo amezungumzia swala zima la mashabiki kuwa na mapenzi zaidi kwa muziki wa nje kuliko wa nyumbani Tanzania na amesema inamuumiza sana maana inauangusha muziki wa Tanzania.

Ungana naye kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo saa 16:00 Jumatatu hadi Ijumaa.

Rapper huyo alitoa ufafanuzi huu kuhusiana na swala zima la mashabiki kupenda zaidi muziki wa nje msikilize.

“Mimi kama msanii ninapata maswali, kwanza inaniumiza, ikidondoka ngoma ya Nigeria yaani ndo habari ya mjini,” Alisema

 “Mifano ndio hiyo Miss Tanzania wanapigia ngoma za Nigeria, kwenye maharusi wanapiga ngoma za nje, hiyo ndiyo inapelekea mpaka mashabiki wanashindwa hata kudondoka kwenye show kwa wingi"

Roma alimalizia "Ni kitu gani au thamani ya msanii imeshuka bongo au watanzania hawana uzalendo hawawezi kupenda cha nyumbani wala kukikubali ama media zimeshawaambukiza mashabiki kwamba vya nje vinathamani kuliko vya ndani.”