Msanii kutoka Tanzania Roma Mkatoliki

Rapper kutoka Tanzania akifahamika kama Roma Mkatoliki ambae anazidi kupanda chati kwa sasa na hit yake mpya alioifanya kwa maadhi tofauti ya kisingeli na kuipa jina K.

Roma amesema ngoma yake K aliyofanya na Baghdad imeongeza idadi ya simu anazopigiwa na mapromota kwa ajili ya show.
 
Kutana na rapper Roma na wimbo wake wa K kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
 
"Wimbo huo umekuja na neema tafauti na watu wanavyofikiria. Kwa upande wa watu wanaoukosoa wimbo huo, Niliamua kubadilika kuwaonesha mashabiki kuwa ana uwezo wa kufanya muziki wa aina mbalimbali," Roma alisema.

Amedai kuwa mapromota wengi wamekuwa na mawazo wa kufanya naye show zenye majina ya wimbo huo. Na pia kuwa hivi karibuni aliitumbuiza ngoma hiyo jukwaani na watu wakapagawa vibaya.

Yasome maoni mengine ya rapper mwingine wa Tanzania Darassa. Amesema nini kuhusu Diamond Platnumz?