Msanii wa hit single Amarulah, Roberto

Msanii Roberto amesema hataisahau 2015 kwa sababu single yake ya Amarulah imemvusha mipaka

Tunamjua msanii anaemiliki hit single ya Amarulah Mzambia Roberto ambaye mwaka 2015 umemuendea vizuri sana kutokana na single yake moja tu hiyo ambayo imemvusha mipaka kwenda kufanya shows.
 
Roberto ameiambia DStv.com ijapokua alishawahi kutoa album nyingine kabla, single ya Amarulah ndio kama imemtambulisha kwa mamilioni ya watu wa Afrika mpaka kufanya aitwe kufanya show Tanzania mara mbili.
 
Sikiliza hii single ya Amarulah na zingine pia kutoka kwa wasanii kama Alikiba, Christian Bella na Diamond Platnumz kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Amesema pamoja na kufanya shows, kitu ambacho hawezi kukisahau mwaka 2015 ni pale alipopigiwa simu na kampuni ya kinywaji cha Amarulah ambayo iliweka wazi mipango ya kufanya nae kazi kutokana na huo wimbo.
 
So far mwaka 2015 umemwendea vizuri kutokana na hit single ya 'Amarulah' lakini ameahidi kwamba mwaka 2016 utakua mwaka wa mafanikio zaidi kwake sababu ameendelea kujua zaidi Afrika inataka nini.
 
Roberto yuko Tanzania kufanya show ya pili kwenye nchi hii ambapo ya kwanza aliifanya Mwanza na ya pili ni hapa Dar es salaam.