Msanii wa bongofleva Rich Mavoko

Msanii wa bongo Rich Mavoko kazungumzia kufanya collabo na Mnigeria

Tunae leo staa kutoka bongoflevani staa wa hit single ya Pacha Wangu, Rich Mavoko, ambaye amekuwemo kwenye list ya wabongo waliopata sana nafasi ya kuchezwa kwenye radio na TV.

Ameongea na dstv.com na kusema yake kuhusu kufanya kolabo na Wanigeria, "Kwangu mimi kwa upeo wangu nataka kutengeneza brand yangu, nitengeneze jina langu kwanza wale watu wa West Africa wajue kwanza kuna kiumbe kinaitwa Mavoko."

Kusikiliza wasanii wengine wanaowakilisha Africa, tazama kipindi cha Africa 10, Alhamisi saa 23:00 kwenye TRACE Urban, ambayo unaweza kutazama kwa Explora, pia kurekodi zile unazozipenda.

Kwenye sentensi nyingine Rich Mavoko amesema na ikitokea siku moja akafanya kolabo na Mnigeria, nafasi ya kwanza itakua kati yake na Wizkid manake ni mkali na anajua kubadilika, unaweza kumuweka kwenye muziki wowote na akabadilika nao.