Diamond and Zari dressed in all white

Mwimbaji wa bongofleva Diamond Platnumz pamoja na girlfriend wake Zari wataangusha White party siku ya kwanza ya May 2015.

Dar es salaam Tanzania itaandikiwa historia nyingine kwenye list ya zile party kubwa zilizowahi kufanyika kwenye jiji hili lenye starehe zake.

Mwimbaji wa bongofleva Diamond Platnumz pamoja na girlfriend wake Zari wataangusha White party siku ya kwanza ya May 2015.

Bab Tale ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz amesema tayari party hiyo imeonyesha mafanikio makubwa kwa kuvunja rekodi ya mauzo ya ticket zake.

Amesema: "Sisi tulikua tunajua tukitangaza zile ticket za milioni 3 basi zitakaa mpaka zichubuke lakini zimetangazwa na zikawa zimenunuliwa ndani ya dakika 180."

"Ni ticket moja inayobeba watu wanne na zilikua kumi tu hivyo zikamalizwa na watu wanaoisubiria hii party na hiyo ilikua ni baada tu ya Diamond kutangaza kupitia page yake ya Instagram."

Party hiyo itahudhuriwa na mastaa mbalimbali wa Tanzania akiwemo Nay wa Mitego, Shamsa Ford, Shetta na wengine.

Kama wataka kuwa na party yako mwenyewe jiburudishe wa Kiafrika kwenye kipindi cha Official African Chart kila Jumanne saa 21:00 kwenye MTV Base.

Related