Msanii Rayvanny kutoka Tanzania

Rayvanny ni msanii kutoka Tanzania ambae yuko chini china ya WCB label inayomilikiwa na Diamond Platnumz na amekuwa akifanya vizuri sana kwenye game kwa kipindi kifupi tu tangu aanze mziki.

Baada ya ujio wa mtoto wa pili wa Diamond na Zari, Raymond kwa sasa yuko South Africa tukifahamu kuwa lengo ni kumwona mtoto lakini kumbe kuna lingine.
 
Dj Maphorisa wa South Africa ni miongoni mwa ma dj wakali sana na wenye umaarufu mkubwa Africa na ameshafanya kazi na wasanii wachache kutoka Tanzania kama Diamond ,Vanessa Mdee na Chegge pia Wizkid wa Nigeria ambae walitikisa na ngoma yao Soweto Baby.
 
Kutana na Rayvanny kwenye kwenye Mziki Hit 10 siku ya Ijumaa saa 17:15 ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Rayvanny amepost picha na video kuonesha kuwa kuna kazi soon ataitoa na staa huyo all the way from SA. Pia Diamond alipost kudhibitisha hili kwa kuandika hivi.
Diamond ameandika kwenye Instagram: @djmaphorisa & @rayvanny about tu Burst your Speakers 🔥🔫 !!!!! #WcbWasafi for Life!