Rayvanny kutoka Tanzania

Msanii wa muziki kutoka WCB, Rayvanny amedai ataachia wimbo wake mpya muda mchache ambapo hivi karibuni ameshirikishwa Queen Darlin kwenye nyimbo inayotamba kwa sasa Kijuso.

Pia uliyaskia ya Rayvanny kuingia studio na DJ Maphorisa kutoka Afrika Kusini. Yote twakuletea hapa.

Rayvanny ambaye bado anafanya vizuri na wimbo Natafuta Kiki amedai ameandaa kazi nyingi ambazo zinasubiri wakati wa kutoka.

Kutana na Rayvanny na ngoma yake Natafuta Kiki kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.

Akizungumza na mashabiki wake live katika mtandao wa Instagram (Insta Live), Rayvanny amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwa ajili ya ujio wa kazi mpya.

“Mashabiki wangu soon nitaachia wimbo mpya, sema itaanza kwanza kutoka video ya ‘Kijuso’ na baada ya hapo ndo mzigo unaweza kutoka,” alisema Rayvanny.

Muimbaji huyo toka aachie wimbo Natafuta Kiki, ameshirikishwa kwenye ngoma zaidi ya 3 ambazo ni pamoja Salome aliyoshirikishwa na Diamond, Kijuso na Queen Darlin pamoja na Mugacherere na Q Boy.

Barnaba naye amesema nini kuhusu ngoma yake mpya? Soma mengi hapa.