Raymond Rayvanny

Rayvanny msanii aliyeingia na kukua kwa kipindi kifupi sana kwenye bongofleva na bado anafanya vizuri zaidi kwenye game hii akiwa chini ya label ya Diamond Platnumz WCB.

Taarifa ikufikie kama wewe ni shabiki wa Raymond (Rayvanny) ambapo leo amezungumzia kuachia collabo mpya na Diamond.
 
Hitmaker huyu wa Natafuta Kiki ambaye siku chache tu amechukua tuzo za Hipipo zilizotolewa nchini Uganda kwa collabo alioshirikishwa na Diamond, Salome.
 
 
Rayvanny amewaweka tayari mashabiki wake kwa ajili ya collabo nyingine tena na Diamond ambapo amesema sasahivi ngoma itakuwa yake yeye.
 
Burudika na hit ya Rayvanny Natafuta Kiki kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
“Lazima,watu wasubiri,” alisema Ray, ikiwa kama hapo awali ambapo wenzake kwenye label hiyo walishafanya ngoma zao na boss wao Diamond na kuhit kama Bado ya Harmonize na Kokoro ya Rich Mavoko.