Msanii wa Tanzania Rayvanny

Leo kutana na msanii aliyekuwa kwa kasi ndani ya mwaka mmoja ambapo nyota yake imekuwa iking'aa zaidi tangu aingie kwenye game ya bongofleva mwaka 2016 chini ya label ya WCB, Rayvanny.

Wasanii hasa wa bongofleva wamekuwa wakituhumiwa kuwatumia wanawake hususan wenye majina makubwa kama njia ya kutafuta kiki ili majina yao yaendelee kuwa mdomoni mwa mashabiki.
 
Hii imesababisha kutokuwepo na imani kwa mashabiki kuwa na mtazamo tofauti katika mahusiano mengi ya mastaa wa bongo na kuonekana kutoaminika kuwa na ukweli katika mahusiano hayo bali hutafsiriwa kama kutafuta kiki.
 
Mengi kuhusu wanawake na wasanii, uliyaskia ya Harmonize na Wolper? Yote yasome hapa.
 
Rayvanny amedai kuwa kwa msanii, mwanamke sio kiki bali ni stress tu. Ray alidai kuwa wanawake wamekuwa wakiwapa zaidi stress wasanii na wengi wakijikuta wakipotea kabisa.

Alidai kuwa uhusiano hasa pale unapoanza kuingia kwenye migogoro humfanya msanii apoteze concentration kwenye muziki wake na kupoteza vingi.

Alitolea mfano hata habari za udaku kuhusu girlfriend wa staa fulani kuhusishwa kuwa na uhusiano na mtu mwingine huwachanganya wasanii sababu huonekana kama wana udhaifu.

Mbali na wanawake na kiki kwenye bongofleva, kutana na msanii Rayvanny akimhusisha Diamond Platnumz kwenye hit ya 2016 ya Salome kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.

Related