Muigizaji wa bongomovie Vincent (Ray) Kigosi

Maadili ya KItanzania yanasababisha tunashindwa kuvaa uhusika kwenye baadhi ya Filamu - RAY KIGOSI

Vicent Kigosi aka Ray ni msanii nguli wa maigizo ya bongomovie ambaye siku sio nyingi ameachia movie yake mpya inaitwa Gatekeeper.
 
Pia tazama bongomovie Kadamanja, siku ya Alhamisi 16 March saa 20:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Ray amezungumzia kuhusu industry ya filamu Tanzani na kusema haya, "Kutokana na maadili yetu kuna baadhi ya movie tunashindwa kuvaa uhalisia tukihofia bodi ya filamu itafungia kazi zetu. Mara nyingi scene za mapenzi sio rahisi mtu kuvaa uhalisia."
 
Ray ameshawahi kufungiwa movie yake ilikuwa inaitwa Sister Mary ambayo alisema ingawa ni mambo ambayo yanaendelea kwenye jamii lakini bado BASATA (Baraza la Sanaa Tanzania ) walifungia movie hiyo kwa madai kuwa inapotosha jamii.