Msanii wa Tanzania Ray C

RAY C AMEYASISITIZA HAYA BAADA YA KURUDI UPYA KWENYE MZIKI

Ray C ama Rehema Chalamila ni kati ya wasanii wa mwanzoni kutokea Africa Mashariki kupokea tuzo za nje ya nchi kama Channel O.  Muziki wake ulimpatia umaarufu ndani na nje ya bara la Africa.

Pamoja na tuzo za (KTMA) Kilimanjaro Tanzania Music Awards, Ray C aliweza kujijengea heshima kwenye soko la muziki Tanzania ukiangalia pia na namna ambavyo hapakuwa na wasichana wengi waliokuwa wakifanya mziki kipindi hicho.

Ilifika kipindi Ray C alistop kabisa kufanya muziki na hii ilipelekewa na yeye kujiingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya hali ambayo ilipelekea kushindwa kuendelea kufanya mziki. 
 
Lakini baada ya kuathirika na madawa alipatiwa matibabu kwa muda na sasa yuko sawa kwa kiwango cha kutengeneza  mziki mzuri ambapo kwa sasa ameachia wimbo mpya unaoitwa Unanimaliza.
 
Burudika na hit hii mpya kutoka kwa Ray C kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Ray C amesema kwa sasa hana mpango wa kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na hatohitaji lakini pia anaamini huu ni wakati muafaka wa yeye kufanya muziki kwani anaona njia nyingi za kufanya vizuri ndani na nje yaTanzania na anachoomba ni support ya mashabiki pamoja na imani yao kwake.
 
Amesema, "Sina mpango wa kuwa kwenye mahusiano kwa sasa, naamini huu ni wakati mzuri wa kufanya kazi, fursa ni nyingi na nina imani nitafanya vizuri nikipata support kutoka kwenu."