Mwimbaji Rachel kutoka Tanzania

Kutana na Rachel, msanii wa Tanzania aliyeziacha dawa za kulevya

Kwenye exclusive ya DStv.com leo tunaye mwimbaji Rachel ambaye uzito wa jina lake ulianza kuongezeka alipoanza kuachia nyimbo zake akiwa nyumba ya vipaji Tanzania THT.

Rachel amemwambia ripota wa DStv Millard Ayo kwamba ameamua kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya aina ya bangi ambayo alikua akiivuta kwa kitambo mpaka kupoteza marafiki.

Pia unaweza kujua mengi kuhusu mastaa wa Tanzania kwenye Inside Bongowood kila Jumanne saa 21:25 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Rachel amesema: "Kiukweli bangi nimeshaacha, kweli nilikua navuta bangi toka nilipotoa wimbo wangu wa pili na baada ya hapo nimekalishwa chini na bosi wangu na familia, nikawasikiliza na sasa nimeacha."

Akaongezea: "Nimepitia mengi kwenye maisha na muziki nahisi hiyo inaweza kuwa chanzo, kuna kipindi maisha yalikua magumu kwangu na nilipoanza kuvuta bangi ndio marafiki wakanikimbia kabisa, dawa za kulevya sio nzuri na sizitaki, kweli baada ya kuacha nimebadilika sana."

Hayo ni maneno ya Rachel ambaye amerudi Tanzania akitokea Oman alikokua amekwenda na kukaa huko kwa zaidi ya miezi saba baada ya kupata matatizo mbalimbali kwenye Visa yake.