Q Chief kutoka Tanzania

Q-Chief ama Q Chillah akiwa kama msanii mkongwe kwenye tasnia ya muziki wa bongofleva Tanzania na bado anahit mpaka sasa hivi na hit song yake ameipa title Sungura.

Kutana na Q Chief kwenye kwenye Mziki Hit 10 siku ya Ijumaa saa 17:15 ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Siku hizi kumekuwa na desturi ya wasanii kuweka bayana mahusiano yao ya kimapenzi wazi kwenye social media zao sio kama hapo awali na Q Chillah ameingia kwenye list ya wasanii hao.
 
Q Chillah ameyatoa ya moyoni kuhusu mpenzi wake ambae anadai kutimiza nae miaka miwili sasa na ameyandika haya kwenye Instagram yake.
 
“Soon tunatimiza miaka miwili katika uhusiano wetu. Umekuwa mvumilivu mwenye hekima, ni wanawake wachache sana dunia hii wenye moyo wa chuma ulionao."
 
Aliendelea, "Tumepita rough roads, tumevuka vikwazo vingi tumepitia kila aina ya changamoto but most important tumepigana vita zote na kushinda sisi ni wababe wa vita love you honey, soon utatoka juani na utajikuta kivulini naamini maana Mungu wetu yu mwema nakizuri zaidi anatupenda sana."