Profesa Jay bungeni

Msanii na mbunge Profesa Jay azungumzia beef bongoflevani na kufafanua kwa nini hakipendi

Legend wa muziki wa bongofleva Profesa Jay amekaa kwenye exclusive na Millard Ayo, ripota wa DStv na kuweka wazi ni vitu gani hapendi kuviona kwenye muziki wa bongofleva sasa hivi.

Anasema: "Mimi sipendi kuona beef ambazo hazijengi, unajua watu wanaiga vitu vingi watu wanaamini kwamba kina 50 Cent wanavyokua na beef na kina Rick Ross basi ndio na sisi tunaweza kufanya Tanzania, no... sio sahihi."

Kutana na Diamond na Alikiba ambao inasemekana wana beef kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160) saa 16:00, Jumatatu hadi Ijumaa.

Anaongezea: "Unaposikia kuna timu flani sijui timu flani kidogo inanizingua, muziki wetu bado unahitaji mshikamano, muziki wetu unahitaji umoja ili tuweze kusonga mbele."

Profesa ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Mikumi ameongezea kwa kusema Wanigeria ukiwasikiliza unaweza kujua wana beef kumbe wale watu wanashikana mikono na wanasaidiana, tufanye hivyo na sisi, kiukweli sipendi beef kuliko chochote.