Peter of P Square

Peter wa P Square aongea kuhusu Diamond Platnumz

Staa wa bongofleva Diamond Platnumz jina lake sio dogo tena kwenye headlines za Afrika, ni mkali ambaye ujazo wa jina lake uliongezeka sana Afrika baada ya kushinda tuzo tatu za Channel O 2014.

Baada ya hapo ikawa sio tabu tena hata ukisema umetoka Tanzania, ni jina ambalo wengi walilishika baada ya vyombo mbalimbali vya habari Afrika kuandika jina la Diamond na Tanzania baada ya ushindi huo wa tuzo tatu ndani ya tukio moja.

Ushindi wa tuzo nyingine ya MTV Africa Music Awards 2015 (MAMAs) ndio umemuweka Diamond juu kabisa na sasa anakaa meza moja na mastaa kama D'Banj, AKA, Mafikizolo, Uhuru na wengine.

Kwa tuzo zingine, usikose kutazama The 67th Primetime Emmy Awards 2015, itakayopeperushwa LIVE, Jumatatu 21 September saa 02:00 kwenye M-Net.

Stori nzuri ya leo ni kwamba Peter wa P Square amethibitisha kwa Afrika kwenye exclusive interview na DStv.com kwenye red carpet ya MAMAs kwamba P Square wamefanya kolabo na Diamond Platnumz nchini Nigeria.

Peter alisema walikiona kipaji cha Diamond toka siku nyingi na wao huwa hawafanyi kolabo kila siku ila wameona ni muhimu kufanya na Diamond hawawezi kumuacha apite hivi hivi.

Peter ameipongeza pia Tanzania kwa kumsupport Diamond na kusisitiza msanii anafanywa mkubwa kuanzia nyumbani kwao kisha ndio anavuka mipaka, kolabo yao imefanywa kwenye studio ya Peter nyumbani kwake na soon itatoka.

Usikose kujiburudisha na tuzo za The 67th Primetime Emmy Awards 2015, itakayopeperushwa LIVE, Jumatatu 21 September saa 02:00 kwenye M-Net.