Msanii wa Tanzania Ommy Dimpoz

Kutoka Tanzania msanii na mmiliki wa label ya PKP Empire akifahamika kama Ommy Dimpoz  amezikamata headlines kwenye page zetu ambae pia ni hit maker wa ngoma yake alioitoa 2016, Kajiandae ft King Kiba.

Burudika na hit hii ya Kajiandae kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Ommy ameongelea muziki ambapo yeye anadai kuwa video nzuri kama wimbo ni mbaya ni kazi bure na amesikika akifafanua hivi. Amedai kuwa wasanii wengi wamekuwa wakiweka nguvu zao zaidi kwenye video bila kuzingatia nguvu ya audio.
 

“Sasa hivi tunatakiwa tofocus kwenye muziki zaidi, yaani kuutengeneza muziki wenyewe zaidi kuliko kufikiria video,” Ommy alizungumza.

Aliendelea, “Video hata iwe nzuri vipi, kama nyimbo ni mbaya haiwezi kukusaidia kitu, lazima kwanza tudeal na audio. Ukitengeneza mzuri hadi wewe mwenyewe unarelax.”

Mengi kwenye bobgofleva, soma aliyosema Darassa kuhusu muziki wake.