Maisha Magic Bongo (160) inakutuza kwa kuwa mtazamaji wetu bora mwezi huu na filamu mpya na za kipekee sana katika mwezi huu wa Oktoba. Na tuangale yapi waliotuandalia. Alhamisi, 6 Oktoba saa 19:00 tunampata Dickson kwenye Msingi Kiuno ambaye inabidi afanye kazi kama gigolo ili kuweza kupata riziki. Je ataweza na maisha ya wasichana? Tazama Maisha Magic Bongo kujua zaidi.

Katika Shobo tunampata predeje Juma ambaye ushauzi anao na mwingi ten asana. Kwa mtu anayefanya kazi ya kuchunga usalama tabia hii haitakikani. Pata vile wenzake watamfunza adabu.Haya yote Alhamisi, 6 Oktoba 19:00.

Siku za mwizi ni arobaini kweli katika Wape Salam Zao. Landlord huyu anapatikana akiwaibia wapangaji wake bila hao kujua. Muda si mrefu wanagundua na kumpangia jama. Jua yatakavyoisha Jumatano, 12 October saa 19:00.

Zindi nayo inatufundisha maisha kitenesi kwa hivo tenda wema uende zako kwani utakachokifanya kitakurudia wewe tu. Jifunze na filamu hii Alhamisi, 20 October at 19:00.