Msanii wa Tanzania Nuh Mziwanda

Kwenye hii post tunaye msanii kutoka bongoflevani Nuh Mziwanda ambaye ameongelelea swala la yeye kufungua studio ambayo ataimiliki yeye binafsi.

Msanii Nuh mmiliki wa hit single ya Jike Shupa aliyomshirikisha Ali Kiba ameelezea kuhusu hiyo ishu ya studio, "Well kila mtu anandoto zake na namshukuru Mungu nimeshaagiza vifaa vyangu vya studio ambavyo vipo Tanzania tayari na nshapata sehemu ambayo ntaiweka iyo studio."

Nuh ameongelea pia jina la studio hiyo na lengo pia ya studio hiyo pia zaidi ameongezea kuwa hit single yake ya Jike Shupa ndio iliyomwingizia pesa atakayofungulia studio hiyo na ameyaeleza haya hapa chini.

Single hii ya Jike Shupa na Ali Kiba inakujia anakujia kupitia Mziki Fresh, Jumatatu hadi Ijumaa saa 20:00 kwenye channel mpya ya TRACE Mziki (323).

Amesema, "Studio hii itaitwa LB Records au Lastborn Records na dhumuni kubwa sana la kufungua studio hii ni kusaidia  wasanii wachanga wanaotaka kutoka kimziki kwasababu mimi najua msanii mpaka uje kutoka unatumia nguvu nyingi sana lakini pia ita deal na mastaa wakubwa ambao nina uwakika wa asilimia mia nnaweza kufanya nao kazi mfano kama Ali Kiba na wengine."

Je, uko na DStv dekoda utazame TRACE Mziki? Jaza fomu hii hapa chini upate dekoda yako kwa urahisi: