Je upo tayari? Msimu wa  sikukuu unakaribia. Mwezi huu wa Novemba tunawaletea vipindi na Tamthilia  za kusisimua katika Maisha Magic Bongo.

Shuhudia safari wa wapendanao kutoka Tanzania pilika pilika zita tutaanzia kwenye  Kitchen party, Sendoff party, na hatimaye harusi  yenyewe zote utazipata kwenye Harusi Yetu kipindi  kipya kabisa, kitakacho letwa kwenu na Salma Msangi na Penniel Mwingilwa yani the hostess with the mostest. Tarehe ni Jumapili, 6 Novemba saa 18:00 CAT kwenye Maisha Magic Bongo.

Riyama Ally, Grace Mapunda, Haji Salum na wengine wengi kwa pamaoja  wanatuletea Tamthilia mpya Huba inayohusu  tamaa ya pesa na mapenzi, usaliti na mengine mengi  katika pilka pilka za Maisha ya mapenzi na ndoa ndani ya Huba . Usikose kushuhudia Tamthilia hii Jumanne na jumatano saa 18:30 CAT.

Kila Jumapili tunawaletea kipindi cha  Sifa Mixx kujumuika na wakristo wote  kusikiliza nyimbo za injili tupate baraka tele . Ungana nasi basi Jumapili saa 11:00 CAT kwenye MMB.

Maisha ya  ndoa ya  Dalmas  imefana lakini mama mkwe na mawifi  wameshindwa kukubaliana na ukweli. Wanahakikisha anaoa mwanamke mwingine. Wanaachana na maisha yao yanabadilika, Je, unahisi nani alijutia? Shuhudia  Ndoa Ya Utata Jumanne, 8 Novemba saa 19:00 CAT kujua

Tunakuletea bonge ya movie hujawahi kusikia  Juma ndiye  Mmbea wa Jiji. Ugombanishi, visa na umbea ndio zake. wamemchoka sana na tabia zake hivyo wapanga kumfunza adabu. Je, watampata na umbea gani? Tazama Maisha Magic Bongo Jumatatu, 21 November saa 19:00 CAT kushuhudia msuto wa

Kwa kumalizia tunawapa hii hapa wapenzi wa  filamu za kihindi. Doli Aramno Ki ndio series itakayo kusisimua, kwani  ndoa ya  Urmi na Samrat itakavyoambulia patupu kwa sababu ya mateso na wivu. Pata kujua nani kamchezea nani Jumapili, 9 Novemba saa 17:00 CAT.