Mwigizaji wa Tanzania Nisha

Salma Jabu mwigizaji staa wa movie mpya ya Kiboko Kabisa, Nisha ameiambia DStv.com kupitia ripota Millard Ayo kwamba amekwenda China kusomea ujasiriamali kwa sababu anataka kuwa mfanyabiashara mzuri.

Ni masomo ambayo yatamchukua muda wa miezi mitatu mpaka kuyamaliza na akirudi Tanzania atafungua duka litakalodili na ishu za harusi pamoja na birthdays.

Sura ya Nisha imeshaonekana sana kwenye filamu kadhaa za Tanzania na hata wale watu wangu watazamaji wa Maisha Magic Bongo walishaiona kwenye movie kadhaa za kushirikishwa ila hajaridhika na filamu peke yake, anataka kutengeneza pesa kwenye njia nyingine pia.
 
Kutana na mastaa wengine wa Tanzania kwenye Jikoni na Marion kila Alhamisi saa 19:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Anasema "Nakumbuka siku nliyofaulu kuendelea form 5 ila ikashindikana sababu ya ada kidogo tu, nakumbuka zaidi siku iliyopatikana ada ila choice ilikuwa nani apelekwe shule kati yangu na mdogo wangu wa kiume,na nikamwambia mama msomeshe mdogo wng sababu yeye ni mvulana mm nitafutie kazi nifanye ntakuja kujisomesha mwenyewe nikifanikiwa Inshallah."


Akaongezea, "Kweli Mungu huwa anasikia kilio cha wengi na hujibu hata akichelewa hujibuleo nafuta machozi ya mama yangu na najisomesha mwenyewe tena nchi ya mbali".

Kijana mwenzangu usikate tamaa,yote unayopitia jua siku moja yataisha,kikubwa fanya jitihada ya unachopenda,usikate tamaa,heshimu mkubwa na mdogo,weka akiba,muombe sana Mungu,penda watu wote. Kingine kuwa mwingi wa kusamehe na kusahau mabaya.