Msanii wa hiphop kutoka Tanzania Nikki wa Pili

Mkali wa hiphop kutoka Tanzania kutokea kundi la Weusi, Nikki wa Pili ambae ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri kwenye mziki wa Hiphop Tanzania ambae kwa sasa anatamba na hit song yake Sweet Mangi.

Kutana na Nikki wa Pili na hit song yake Sweet Mangi kwenye Mziki Hit 10 saa 17:15 kila Jumatano ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Tunafahamu kuwa kumetokea headlines za kutolewa kimakosa kwa tuzo za MTV EMA kwa kupewa msanii wa Nigeria, Wizkid na baadae kutajwa kuwa mshindi halali ni Alikiba kutoka Tanzania ndipo tuzo hiyo kurudishwa kwa Alikiba.
 
Msanii Nikki wa Pili ameingia kwenye headlines baada ya kuzungumzia MTV EMA kuhusiana na makosa hayo yaliofanyika kuwa ni makosa kama makosa mengine tu watu wanayofanya.
 
Nikki alizungumza haya, "Mimi nadhani walikosa umakini lakini pia kukosea ni kitu cha kawaida as long as waligundua wamekosea na wakafanya kitu sahihi so me sioni kama kuna tatizo."
 
Nikki alimalizia, "Kosa walilolifanya limeonesha kuwa wao pia ambao wanatazamiwa kuwa na umakini wa hali ya juu nao hukosea kama wengine."