Msanii rapper Joh Makini

Baada ya kusikia zile stori nyingi kuhusu ushirikiano wa rapper wa Tanzania Joh Makini na mwimbaji wa Nigeria Davido, time imefika ya kupewa tulichokitarajia.
 
Ukweli ni kwamba wawili hawa wameshakutana South Africa na kufanya video ya kolabo yao matata na tayari wameshamaliza uchukuaji picha wa video yao mpya ambapo Davido ndio kashirikishwa.
 
Kutana na Joh Makini kwenye Mziki Hit 10, kila Ijumaa saa 17:15 ndani ya TRACE Mziki (323).

Kwenye exclusive na DStv, Joh amesema, "Hakukuwa na ugumu wowote kufanya kazi na Davido na yeye tayari alikua na vibe ya hatari, kumbuka kwamba yeye ndio alinicheki mimi ili kufanya kazi, yeye mwenyewe alikua na mzuka na kufanya kazi na mimi."

Mbali na Davido, msanii mwingine ambaye angependa kufanya kazi na Joh Makini ni Rayvanny. Soma mengi hapa.

Aliongezea, "Production imefanywa na Nahreel na kabla ya mimi kukutana na Davido tulishaifanya audio, hatukuingia studio pamoja bali tulitumiana zile voco kupitia mtandao na mambo yakajipa."

"Siwezi kutaja jina la ngoma yenyewe kwa sasa lakini nakwambia ngoma zangu zote ni kali na hata ukiniuliza ni ngoma gani kali kuliko nyingine siwezi kukujibu sababu kila ngoma ina historia yake, nafanya vitu tofauti na hiyo ni dhamira ya Weusi."

Joh alimalizia, "Sio tu kolabo na Davido, nina kolabo nyingi na wasanii wa kimataifa na mashabiki wanipe time tu nitaziachia na zinazidi kunikuza sana, kama ile na A.K.A imeniletea heshima."