Msanii wa bongofleva Snura

Msanii wa bongofleva Snura atuelezea mengi kuhusu maisha yake.

Tunao mastaa wengi sana ambao hutuonyesha kila kitu kwenye Instagram, Twitter ama Facebook lakini unajua kwa nini Snura Mushi hakutuonyesha akiwa mjamzito?

Well, kama ulikua hujui staa huyu wa hit single ya Majanga alipata mtoto wa pili hivi karibuni lakini ilikua suprise manake ni ndugu zake tu ndio walikua wanajua ni mjamzito, tofauti na hapo hakuweka chochote kwenye mitandao yake ya kijamii.

Baada ya kuongea na dstv.com Snura amesema: "Niliamua kutoutangaza ujauzito wangu sababu mimba sio matangazo, mimi ni mtoto wa Kiislamu nadhani Wanawake wenzangu wananielewa."

"Vilevile nilifanya hivyo kwa makusudi kama suprise kwa mashabiki wangu, nashukuru Mungu nimekuja kumuonyesha mtoto wangu hadharani na hawakukasirika, nilitegemea wangekasirika lakini sio hivyo," asema Snura.

Kwenye picha hapa unawaona watoto wake wawili, mkubwa wa kwanza na huyu wa mwisho aliezaliwa hivi karibuni.

Sasa hivi Snura yupo kwenye airwaves na single yake mpya ft.Nay wa Mitego iitwayo Hawashi.

Related