The cast of Sweet and Sour

Tazama mapenzi ya Piya na Suhaan kwenye filamu ya Bollywood Jaaneman na burudani mengi kwenye Maisha Magic Swahili.

Kama kawaida hii wiki, unaweza tazama series na filamu ambazo unapenda katika Maisha Magic Swahili. Tunazingatia baadhi ya filamu ambayo haufai kukosa kutazama katika, na ni kwa nini:

Ubaya
Alex ni kijana tajiri na mwenye ukarimu. Mashemeji wake Zubeda na Chadi wanamfanyia yeye kazi, lakini siku moja wanafanya kitendo ya kushangaza huku wakijaribu kumharibia kazi. Director Deogratius Shijaa anawashirikishisa wahusika: Njuma Mrisho, Happy Jamhuri na Tully Mwaisaga.
Tazama Ubaya Friday, 13 March saa 19:00 CAT.

Jaaneman
Ni filamu ya kuigiza ya mapenzi kutoka Bollywood. Producer Sajid Nadiadwala na director Shirish Kunder wanawashirikisha wahusika wenye kipaji kutoka Bollywood kama Salman Khan, Akshay Kumar na Preeity Zinta.

Wakati Piya na Suhaan wanakutana chuoni wanapendana na kuamua hakuna kitu kinaweza watenga, ata kama ni wazazi wake Piya. Wanatoroka na kuoana kisiri wakifikiri ya kwamba mambo yao yatafaulu. Hata hivyo mambo yanaharibika wakati Suhaan anapata kazi ambayo inamlazimu kutokua na mpenzi. Je, atamwacha Piya peke yake?
Tazama Jaaneman Saturday, 14 March saa 19:00 CAT.

Sweet & Sour
Baada ya kufiwa, Mzee Benson ana watoto watatu. Mjane Mrs. Fernandes pia ana watoto watatu. Wanapokutana wazee hawa wanapendana na kutaka kuishi pamoja kwa maisha yao ya kuendelea. Lakini watoto wao wanaleta shida kwa sababu ya chuki. Hii ni mchezo wa kuigiza na ya kuchekesha mno kutoka director Sameer Srivastava wa Pilipili Entertainment akiwashirikisha Ahmed Olutu, Techla Mjata na Abdallah Mkumbilla.
Pata kuona Sweet & Sour Sunday, 15 March saa 19:00 CAT.

Hii wiki katika Maisha Magic Swahili endelea pia kujiburudisha na kutazama vipindi vingine kama Taxi Driver na Mashariki Mix Season 4.

Ukitaka bonge la kiburudisho, tazama Maisha Magic Swahili.

Related