Msanii wa bongofleva Shetta

Shetta akataa madai ya kulala chumba kimoja na mwigizaji Rose Ndauka.

Tumekua tukishuhudia skendo mbalimbali za mastaa kwenye magazeti na mitandao mbalimbali ambapo hata Tanzania siku hizi stori kama hizi hazikosekani.

Kwenye headlines ni msanii wa bongofleva Shetta na mwigizaji Rose Ndauka ambao walidaiwa kulala chumba kimoja kwenye hoteli walipokwenda kwenye msiba Morogoro.

Shetta anasema sio kweli kwamba walilala chumba kimoja, kilichotokea ni kulala kwenye hoteli moja na ni kitu cha kawaida sababu alimpa Ndauka lift kwenye gari lake kwenda kwenye msiba.

Kupata habari zingine kuhusu mastar, tazama kipindi cha E! News kwenye E! Entertainment, Wednesday 22 April saa 17:00.

Kilichotokea baada ya hapo ni ndoa ya Shetta kuvunjika, mke wa Shetta ambaye wamepata nae mtoto mmoja ameondoka nyumbani kwa zaidi ya wiki moja sasa hivi akisema hataki tena kuishi na Shetta, anataka talaka.

Shetta ambaye sasa hivi yuko kwenye headlines na hit single Shikorobo amesema bado hajakata tamaa, japo ameendelea kumfata mke wake na akawa hataki kumuona, amesema watu wazima wameingilia kati sasa hivi na kuna matumaini kwamba kila kitu kitakua sawa.