Nay wa Mitego Bongo Star Tanzania

Nay wa Mitego ambaye ni msanii aliyepata umaarufu Tanzania kwa nyimbo zake za kuwachana watu na kuwataja majina ameongea kwanini hana urafiki na Wasanii wengi wa bongofleva.

Kwenye Exclusive Interview na DStv.com Nay amesema "Watu wengi huwa wananizungumzia vibaya juu ya hiki kidogo nilichonacho, wapo wengine ni baadhi ya Wasanii wa bongofleva".

"Sababu nyingine ambayo ndio inanifanya sitaki ujamaa sana na Wasanii maana wengi tunakuwa Wanafiki, sasa hivi tumekaa pamoja utaona ni washkaji alafu ukiondoka tu wanaanza kukusema vibaya"- Nay

 Mengi ya mastaawa bogno na maisha yao pia unaweza kuitazama kwenye Inside Bongowood, Jumanne saa 15:30 kwenye Maisha Magic Bongo.

Nay anasema time yake nyingi amekua akiitumia studio kutengeneza nyimbo zake tu, hana starehe ya ajabu ambayo inaweza kumfanya amalize pesa... hanywi pombe, hatoki sana kwenda viwanja... starehe yake yeye labda ni magari.

Nay wa Mitego anakaribia kuachia single yake mpya baada ya ile ya 'shika adabu yako' ambayo humo ndani aliwataja mastaa kadhaa wa bongo wakiwemo wa movie na bongofleva.