Msanii Nay wa Mitego

DStv yakutana na Nay wa Mitego

Katika nyimbo za bongofleva zilizo-trend au kuzungumziwa baada ya kuachiwa, Shika Adabu Yako ya Nay wa Mitego imo pia ambapo ndani yake amewachana baadhi ya mastaa kama mwigizaji Ray, Wema na Ommy Dimpoz.

Burudika na Nay wa Mitego, Ommy Dimpoz na wasanii wengine kwenye Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.

Nay wa Mitego kwenye exclusive interview na DStv.com amesema, "Kuna matukio yameniandama na inaonekana kama maisha yangu yamekuwa hatarini, niliwahi kufatwa kwa gari usiku na watu nisiowajua lakini hawakunikamata."
 
"Juzi nimepasuliwa kioo cha gari baada ya kushuka kuingia stationary, nilipotoka sikuona mtu yeyote lakini kioo cha nyuma cha gari yangu kilipasuliwa chote na sijakamata mtu mpaka sasa."
 
Kufuatia kuona matukio haya ya kumkosesha amani, mama mzazi wa Nay amemuomba mwanae rasmi aache kuimba au kutoa nyimbo za kuwasema watu maana anaamini hizo ndio zinaleta uhasama au kusababisha yeye kuwindwa.
 
Nay ameiamba DStv.com kwamba anafikiria lakini hajafanya maamuzi bado ila anafikiria kufuata ushauri wa mama yake mzazi kuacha kutoa nyimbo zinazowasema au kuwadiss watu na maisha yao.
 
Ukiburudika na Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo pia unaweza kuitazama vipindi kem kem kwenye Catch Up kwenye DStv Now ama Explora yako. Jaza fomu hii kupata Explora na pia Zapper decoder kwa urahisi: