Nay wa Mitego ni rapper maarufu sana kutokea Tanzania na anafanya vizuri sana kimziki na ambaye sasahivi anatamba kivingine na hit song yake mpya Sijiwezi.

Nay amekuwa ni rapper au miongoni mwa wasanii wanaotoa nyimbo zenye maudhui ambayo wanatoa nyimbo zenye ujumbe wa mapenzi kwa nadra sana na kwasasa Nay ameingia kwenye headlines baada ya kuja na mdundo wake mpya wenye maudhui ya mapenzi tu.

Pata ushauri wa Mama Nay haswa kihusu mziki wake hapa. 

Mashabiki wengi kujiulia maswali nini kimemsukuma rapper huyo kutokana na nyimbo ambazo amefululiza kuzitoa kuwa sio za mapenzi mara nyingi mfano Hapo Kati, Sina Muda na Shika Adamu Yako, za msanii huyo. Nay ametoa sababu kilichomsukuma kuamua kuandika nyimbo mapenzi sasahivi...

“Mimi siwezi kuandika wimbo wa mapenzi bila kupata feeling ya mpenzi kutoka kwa mpenzi wangu au watu wangu wa karibu ndio maana hata unaona na nyimbo chache sana za mapenzi,” alisema Nay.

 Akanendelea kusema: “Hata Sijiwezi umetokana na maisha yangu ya ndani na mpenzi wangu. Nikaona hapa kuna sababu ya kuandika kitu na kweli nimefanya na namshukuru Mungu ngoma inaenda”.

Kutana na wasanii hawa kutoka Tanzania Nay, Jux na Diamond kwenye na mziki yao fresh kwenye Mzooka ndani ya Maisha Magic Bongo (160), Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00.