Group kutoka Tanzania  Navy Kenzo

Ukitaja makundi yanayofanya vizuri Tanzania miongoni mwa kundi bora na lenye mafanikio makubwa uwezi kuacha kuwataja Navy Kenzo ambao pia walikuwa nominated kwenye tuzo kubwa za MTV MAMA 2016.

Kwa sasa hivi Navy Kenzo wameshatimiza kati ya mambo ambayo waliahidi kufanya kama kusaini wasanii kwenye label yao ya The Industry na tayari wamefanikiwa kutoa kazi za wasanii wawili kutokea kwenye label yao.
 
Mbali na hayo, Navy Kenzo pia wametangaza kuachia album yao soon iliyobeba jina la Aim.
 
Waliandika kwenye Instagram, '“Kama tulivyohaidi Desemba hii tutatoa album, tungependa kushare na wewe Official album Cover ya AIM Above Inna Minute #Aim ambayo itakuwa ni album yetu ya kwanza official kutoka kwa Navy Kenzo."
 
 
Kutana na Navy Kenzo kwenye show ya Bongo 10 kila Ijumaa saa 20:00 ndani ya Trace Mziki (323)