Wasanii kutoka Tanzania Navy Kenzo

Ni waimbaji wa hit single Kamatia ambayo imeshika kwenye airwaves za Afrika Mashariki tangu Januari na kuwapa maarufu Tanzania na hata nchi zingine za Afrika. Wasanii hawa wawili Navy Kenzo sasa wamezungumza kwenye exclusive na kuelezea ni nini kinachowaimarisha kimziki bila kusahau tuzo lao la MAMAs ambapo wameteuliwa kwenye category ya Best Group. Wanagombea tuzo hili na Sauti Sol (Kenya), Mi Casa (South Africa), R2bees (Ghana) na Toofan (Togo).

MTV Africa Music Awards itapeperushwa moja kwa moja siku ya Jumamosi 22 Oktoba saa 21:00 CAT kwenye MTV Base (322).

Pia Nahreel amezungumzia kufanya kazi na Diamond Platnumz kwa wimbo wake wa Nana na kutoa shukrani zao kwa TRACE Mziki. Hayo na mengine mengi yasikilize kwenye video hii hapa chini: