Mo Music kutoka Tanzania

DStv.com inae msanii kutoka bongoflevani ambae mnafahamu kama Mo Music, msanii ambae anafanya vizuri kwenye game sasa hivi na hit song yake Ado Ado chini ya Kwetu Studio.

Burudika na hit single hii kwenye show ya Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Mo Music ametaja msanii mkongwe kwenye game ya bongoflevani ambae angetamani arudi kwenye game pia kufanya nae kazi zaidi ameongelea pia msanii anaemkubali wa sasa kwenye game.

 
Amesema, "Natamani sana Marlow arudi kwenye game, ni kati ya watu ambao wamekuwa wakini inspire sana."
 
Alieendela, "Nilipata mazungumzo nae ili tuweze kufanya kitu na tukakubaliana lakini nafkiri hapa katikati vitu havikwenda sawa na sikuweza kuwa tena na contact nae ila ni hivo na wish arudi Malow."
 
Msanii alimalizia, "Umh..msanii namkubali ambae yuko kwenye game ni mwanangu Belle 9, Mr Blue kwakeli napenda kazi zao na waendelee kuwepo kwenye chat zao."