Msanii Raymond Rayvanny kutoka Tanzania

Rayvanny ni msanii kutoka bongo ambaye jina lake linazidi kuwa kubwa kadri siku zinavyokwenda huku akijinyakulia mashabiki sio ndani tu ya Tanzania bali hata nje. Akiwa kama msanii ambaye hana muda mrefu sana kwenye game ya mziki wa bongo.
 
Rayvanny alianza mwaka 2017 vizuri kabisa na hii ni baada pia ya kituo kikubwa cha televisheni cha MTV Base kumtaja kuwa katika list ya wasanii wakutazamwa zaidi mwaka 2017 pamoja na Ben Pol tu wakiwa wasanii pekee kutoka Tanzania.
 
Kutana na Rayvanny kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)
 
Ray alisema kwa sasa anatamani kufanya kazi na wasanii wa nje na pia ameshafanya collabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria na kila kitu kiko tayari ikiwa imebaki tu kuachia nyimbo yao japo hakumtaja msanii huyo kwa jina. 
 
Pia Rayvanny alisema anatamani sana kufanya kazi na rapper Rosa Ree mwenye hit ya One Time kutoka kwenye label ya The Industry iliyoko chini ya kundi la Navy Kenzo.
 
"Unajua Rosa Ree ni kati ya wasichana wanaofanya vizuri sana kwa sasa na ninafikiri nikichanganya mziki wangu na wake tutatengeza moto aisee."