Msanii wa bongofleva Naj

Msanii wa bongofleva Naj awataja wasanii anaowapenda

Sasa hivi idadi ya wasanii wa kike wa bongofleva wenye makazi Dar es Salaam imeongezeka baada ya Mtanzania Naj kurudi kutoka Uingereza alikokua akiishi miaka yote.

Pamoja na mengine yanayoendelea, Naj amesema toka ameanza kuwa shabiki wa bongofleva, wafuatao ni baadhi ya Wasanii ambao hawajawahi kumuangusha, ambao ni Belle 9, anazipenda pia nyimbo za Matonya, Diamond Platnumz, Habida wa Kenya na Vanessa Mdee.

Patana na wasanii hawa kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Naj ameongea na dstv.com na kusema sasa hivi Watanzania pia waisubiri kolabo yake na Jose Chameleone wa Uganda ambaye wameshaongea na kila kitu kiko kwenye mstari.
 
Kwa upande mwingine, Naj amesema ikitokea ikabidi afanye kolabo na Mr. Blue ambaye ni mpenzi wake wa zamani, atafanya tu sababu hamna uadui kati yake bali wamebaki kuwa marafiki.