Msanii wa bongofleva MwanaFa

Msanii wa bongofleva MwanaFA afafanua mengi kuhusu kutaka kuoa anapokutana na mic ya DStv.

Hii ilikua ni exclusive interview pale mwanahiphop staa kutoka bongoflevani MwanaFA alipokutana na Millard Ayo Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano kwenye dstv.com.

Ni staa wa hit single ya Bado Niponipo ambayo mwanzo mpaka mwisho ilikua inazungumzia msimamo wake wa kukataa kuoa kwa wakati huo sababu ya warembo ambao sio waaminifu.

Kusikiliza wasanii wengine wanaowakilisha Africa, tazama kipindi cha Africa 10, Alhamisi saa 23:00 kwenye TRACE Urban, ambayo unaweza kutazama kwa Explora na kisha urekodi zile unazozipenda.

Mapya aliyoyasema MwanaFA ambaye ni baba wa mtoto mmoja. Mungu akijali ataoa ndani ya mwaka mmoja kutoka sasa japo hajaweka wazi ni nani anaetarajiwa kuwa mke.

"Haiko mbali, wakati unafika lakini pia sitaki kuoa kwa presha za watu... nataka kuoa kwa sababu mwenyewe nimeona nataka kuoa, pengine unaweza kuwa umepata mtu  lakini unataka kumtengenezea mazingira asifike mahali akukwamishe."

Hayo ndio maneno ya MwanaFA ambaye anatarajia kuachia single yake mpya inaitwa Sitoi Hela ambayo imefanywa na producer Marco Chali wa MJ Records.

Pia, usisahau kutazama muziki unazozipenda kutoka East Africa kwenye Maisha Magic East itakoyokuja kwenye DStv Channel 158 kuanzia 1 June.