Banners of DStv channels at the MultiChoice showcase in Mauritius

Kwenye MultiChoice content showcase, uongozi wa MTV Base yatangaza kuwepo kwa chati ya muziki wa Afrika Mashariki tu kuanzia 2016.

Ripota wako wa dstv.com nimeyapata mengi sana kwenye tamasha la MultiChoice lililoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kufanyika nchini Mauritius.

Kwenye moja ya press conference, stori ilihusu kituo cha TV cha MTV Base ambacho kimekua kikubwa kila siku kwenye utoaji wa burudani.
 
Uongozi wa MTV Base mbele ya waandishi wa habari Mauritius umetangaza kwamba kuanzia mwaka 2016 kutakua na chati ya muziki wa Afrika Mashariki tu.
 
MTV Base ambayo ni channel namba 322 kwenye DStv itakua inaonyesha video za Afrika Mashariki tu kwenye top 10 kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi na Rwanda.
 
Chati hii itasaidia kupromote zaidi nyimbo za Afrika Mashariki kwa upana na kuzionyesha kwa Waafrika wengine.
 
Tayari wasanii wa Afrika Mashariki wameonyesha uwezo na kuingia kwenye headlines za MTV Base ikiwemo kwenye tuzo za MAMAs ambako Diamond Platnumz alishinda na kuperform pia Sauti Sol wa Kenya.
 
Mpaka sasa wasanii wa Tanzania wanaochezwa MTV Base ni pamoja na Vanessa Mdee, Ali Kiba, Diamond, Navvy Kenzo, Jux na Joh Makini.