Miss Tanzania Lilian Kamazima

Kutana na Lilian Kamazima, mrembo atakayewakilisha Tanzania kwenye Miss World 2015

Ni mwaka mwingine tena wa shindano la urembo wa dunia, wanakutana warembo kutoka kona nyingi za dunia kwenye shindano la Miss Word 2015.
 
Tanzania inawakilishwa na Lilian Kamazima kwenye shindano la mwaka huu litalofanyika December 19 2015 huko Sanya, China.
 
Lilian Kamazima ndio mrembo anayeshikilia taji la Miss Tanzania na imethibitishwa na kamati ya Miss Tanzania kwamba atakuwa mmoja wa warembo zaidi ya 120 watakaoshiriki fainali hizo.
 
Lilian pamoja na wengine watapokelewa China 21 November na kambi yao itakuwa kwenye mji wa Sanya kwa muda wote mpaka siku ya fainali 19 December.
 
Pia kutana na mrembo bingwa Tyra Banks kwenye kipindi cha America's Next Top Model, ambapo models wanapigania nafasi ya kwanza kwenye Vuzu saa 16:00, kila Ijumaa.

Kingine kikubwa cha kufahamu ni kwamba kama Mtanzania unaweza kumpa support kubwa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Twitter, Facebook na Instagram ambazo zitatangazwa soon ili imsaidie kusogea kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuibuka na ushindi wa Miss World 2015.