Trace winner Nalimi Mayunga during an interview with DStv.

Ni nini Akon alimwambia mshindi wa Airtel Trace Music Star Competition? Nalimi Mayunga asema yote.

Fainali ya mashindano ya Trace Music Stars 2015 ilifanyika 18 April Nairobi Kenya ambapo Tanzania ndio iliuchukua ushindi na kuzishinda nchi nyingine 12 za Afrika zilizoshiriki.

Moja ya makubaliano kwenye mkataba wa mshindi ni kufanya kazi na Akon, mwimbaji staa wa duniani ambaye pia alikua mmoja wa majaji kwenye fainali yenyewe.

Jibambe na muziki moto moto za Kiafrika kwenye kipindi cha Official African Chart kila Jumanne saa 21:00 kwenye MTV Base.

Mtanzania Nalimi Mayunga ambaye ndio alichukua ushindi ulioambatana na mkataba wa milioni 900 za Kitanzania ambazo ndio zitatumika kama gharama za kufanya video na audio ameyaongea mengine kwenye exclusive na dstv.com.

 

 

Mayunga amesema Akon amemuhakikishia kwamba kama hiyo single moja wanayotakiwa kuifanya kama mkataba unavyoeleza itafanikiwa, kuna uwezekano akamchukua na kufanya naye kazi ya album nzima, kitu ambacho Mayunga hakutarajia kabisa ndio maana ameahidi kukaza.

Kingine kikubwa alichosema ni kwamba sasa hivi ndio anajiandaa na safari ya kwenda Marekani atakakokaa kwa wiki kadhaa kwa ajili ya kurekodi.

Kama ulikua hujui, Mayunga aliwahi kufanya kazi za kuuza nguo za kike alipoingia tu Dar es Salaam mwaka 2010 kuanza maisha, aliifanya hiyo kazi kwa mwaka mmoja Kinondoni, Dar es Salaam.