Mtanzania Msechu

Peter Msechu ni miongoni mwa waimbaji wa Tanzania waliotajwa sana kutokana na ushiriki wake kwenye mashindano makubwa kama Tusker Project Fame na Bongo Star Search.

Pia, ungana na Watanzania wengine kwenye Tecno Own the Stage, Jumapili saa 18:30 kwenye Maisha Magic Bongo.

Kilichomleta kwenye DStv.com leo ni maamuzi yake mapya na kuukubali ukweli kwamba hawezi kuandika nyimbo bali anahitaji kuandikiwa na kwamba siku zote amekua hafanyi vizuri sababu hiyo.

Kwenye exclusive na DStv.com, Msechu amesema ameshagundua tatizo lililomfanya ashindwe kuingia kwenye Top 5 ya nyimbo bora za bongofleva, kwamba alikua akiandika nyimbo vibaya na hata kuziimba.

"Sasa hivi kazi yangu itakua ni kununua nyimbo na kuzifanyia kazi, siandiki mashairi hata kidogo.... ndio maana hata wimbo wangu mpya wa Malava umeandikwa na Barnaba na akaniandalia kila kitu nikapita nacho" - Msechu
 
Walionishauri haya yote ni pamoja na Kidumu, Boss Ruge na hata Ditto... kwamba ninajua kuimba vizuri sana lakini nyimbo zangu hazina mpangilio, yani hiyo kazi kwa kifupi niachie wengine mimi nibaki kuimba tu na ndio mipango yangu mipya, 2016 kazi itakua hiyo na kuendelea.